DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 23 AGOSTI, 2026 SIKU YA BWANA YA 12 BAADA YA UTATU NENO LINALOTUONGOZA NI:
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni:Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 16/08/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
- Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 16/08/2026 ni Washarika 654 na Sunday School 237
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi na walezi kuwa mazoezi Ya mikaeli na watoto yanaendelea kila Jumamosi. Muda, kwa ibada ya kingereza ni saa 3:00 hadi saa 6:00 mchana, na ibada ya Kiswahili ni saa 6:00 hadi saa 8:00 mchana.
8. Kwaya ya Umoja inaendelea na mazoezi ya Reformation kila Jumanne na Jumatano saa 11:00 jioni. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kwa wakati.
9. Vitabu vya Ibada ya nyumba kwa nyumba vinapatikana dukani.
10. Shukrani
Jumapili ijayo tarehe 30.08.2026 katika ibada ya tatu Familia ya Christina Paul Kibona itamtolea Mungu sadaka ya shukrani kwa kumponya Christina baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa Scitical pain, Pia Binti yake Dr. Chrisha Imani kwa kumbukizi ya kuzaliwa tarehe 28.08.2018
Neno Yer 33:3 na wimbo namba 257 Haya ee moyo wangu
11. NDOA. Ndoa za Washarika
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 04.09.2026
SAA 8:00 MCHANA
Bw.Issaya Y. Igosi na Bi Johary T. Kilagwa
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Itafanyika Kanisani siku ya Jumamosi saa 1:00 kamili asubuhi.
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: kwa Bw & Bibi Salewi
- Madale, Goba, Mivumoni: kwa Bw & Bibi Lawrence Mlaki (Mh. Diwani )
13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya azaniafront. or.tz, pia tupo Facebook na Instagram.
14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki
- | Ndoa |
