DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 11 OKTOBA, 2026
SIKU YA BWANA YA 19 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI:
“ IMANI YENYE USHINDI’’
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni:Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti:
3. Matoleo ya Tarehe 04/10/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
- Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 04/10/2026 ni Washarika 714 na Sunday School 257
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=
7. Kwaya ya Umoja watashiriki Uimbaji ngazi ya Dayosisi awamu ya kwanza leo katika Usharika wa Kipawa. Tuwaombee.
8. Kwaya ya Agape wanawashukuru sana washarika wote waliojitoa na wanaendelea kuungana nao katika kupata pikipiki 10 zitakazoenda Missioni ya Tabora Mungu awabariki. Mpaka sasa zimepatikana pikipiki 5 wanaendelea kuwaomba Washarika kuungana nao ili kufikia lengo. Changia kupitia Akaunti 013874006021 Agape Azania Front au fika Ofisi ya Usharika kwa Mhasibu au ukamuona kiongozi wa Kwaya ya Agape.
9. Viongozi wa Jukwaa la wanaume waliochaguliwa na waliomaliza muda wao watakuwa na mkutano Alhamisi tarehe 15.10.2026 hapa Kanisani. Viongozi wote mnahimizwa kuhudhuria bila kukosa.
10. Uongozi wa Umoja wa Wanawake Azania Front Unapenda kuwatangazia Washarika wanawake wote kujiandikisha katika Umoja wa Wanawake (UWA) kupitia fomu zitakazogawiwa leo. Dhumuni la kujiandikisha ni ili kuwatambua na kushirikiana kwa pamoja kufanya majukumu yetu katika Kanisa,Kujengana Kiroho na kudumisha Upendo na Amani kwa Wanawake wote na Usharika kwa Ujumla. Tunaomba kila mwanamke ajaze fomu na kurudisha leo leo.
11. Jumapili ijayo ya tarehe 18.10.2026 ni Sikukuu ya mavuno. Washarika tujiandae kumtolea Mungu mavuno kwa moyo wa kupenda.
12. Vitabu vya Ibada ya nyumba kwa nyumba vinapatikana dukani.
13. NDOA. Ndoa za Washarika
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 31.10.2026
SAA 9:00 ALASIRI
- Bw. Arnold Charles Mkony na Dorothea Erasmus Mbosha
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
14. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Itafanyika Kanisani siku ya Jumamosi saa 1:00 kamili asubuhi.
- Tegeta,Kunduchi,BahariBeach,Ununio,Boko:Kwa Bw & Bibi Mwemezi Mutembei
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bibi Kelvin Matandiko
- Upanga: Kwa Familia ya Munisi
- Madale, Goba, Mivumoni: kwa Eng. Godfrey Mosi na Dr. Irene Mhalu
15. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya azaniafront. Or.tz, pia tupo Facebook na Instagram.
16. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki
