Alhamisi asubuhi tarehe 30.07.2026;
Ezra 10:11-12
11 Sasa basi, ungameni mbele za Bwana, Mungu wa baba zenu, mkatende alipendalo; mkajitenge na watu wa nchi, tena na wanawake wageni.
12 Ndipo mkutano wote wakajibu, wakasema, kwa sauti kuu, Kama ulivyosema katika habari yetu, ndivyo vitupasavyo kutenda.
Mungu hupendezwa na moyo wa toba;
Israel walikuwa wametoka uhamishoni, kosa mojawapo ambalo waligundua walikuwa wamelifanya ni kuoa wake toka makabila mageni na kuiongezea hatia Israeli. Kwao ilionekana dhambi. Ndipo katika somo la leo asubuhi Ezra anawaita watu kuungama mbele za Bwana na kujitenga na hao wake wageni. Mkutano mzima waliitika, wakawa tayari kutenda hivyo.
Sasa hapa hatujadili ni mke gani wa kuoa, hiyo imeandikwa kuonesha sehemu tu ya historia ya Israeli katika safari ndefu ya Mungu kuwaokoa watu wake. Ujumbe tunaoupata ni Israeli kuwa tayari kuungama kama walivyoelekezwa na Ezra. Nasi tutubu dhambi zetu wakati wote, Yesu anangoja kutusamehe daima. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
