AZF | Mkesha wa Kusifu na Kuabudu (Night of Praise 2024)
Siku ya Ijumaa tarehe 04 Oktoba 2024, ulifanyika mkesha wa kusifu na kuabudu (night of praise) katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral. Tukio hili la kipekee na la aina yake ambalo limefanyika kwa awamu ya pili chini ya uratibu wa Umoja wa Vijana wa Usharika, liliongozwa na Mchungaji Joseph Mlaki na kuhudhuriwa na washarika na wageni mbalimbali.
