April 2022
Ratiba ya Ibada za Pasaka - 2022 @Azania Front Cathedral
Hii hapa ni ratiba ya matukio na Ibada zote kuelekea Sikukuu ya Pasaka ya mwaka huu wa 2022. Nyote mnakaribishwa kujumuika nasi katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral ili kuadhimisha siku hii muhimu katika maisha ya Kikristo. Amen.

Matangazo ya usharika tarehe 10 April 2022
MATANGAZO YA USHARIKA
LEO TAREHE 10 APRIL, 2022
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
HOSANA NDIYE MBARIKIWA, AJAYE KWA JINA LA BWANA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.
3. Matoleo ya Tarehe 03/04/2022
4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Walawi 14:21-32 - 09-04-2022
Yeremia 46:27-28 - 08-04-2022
Luka 7:40-44 - 07-04-2022
Yohana 12:44-20 - 06-04-2022
Walawi 16:29-25 - 05-04-2022
Zaburi 2:1-4 - 04-04-2022
Ibada ya Wazee - Azania Front Cathedral
Siku ya Jumamosi tarehe 2 Aprili 2022 imefanyika ibada ya wazee katika Usharika wa Kanisa Kuu Azana Front Cathedral, jijini Dar es Salaam. Ibada kama hii huwa inafanyika baada ya kipindi maalum ili kuwapa fursa wazee ambao mara nyingi hushindwa kufika kanisani kutokana na sababu mbalimbali hususani zinazotokana na umri wao kuwa mkubwa.
