VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
2 Wafalme 17:34-39

Ijumaa asubuhi tarehe 09.10.2026;

2 Wafalme 17:34-39

34 Hata siku hii ya leo hufanya sawasawa na kawaida za kwanza; wala hawamwogopi Bwana, wala hawazifuati sheria zao, wala hukumu zao, wala ile torati, wala ile amri Bwana aliyowaamuru wana wa Yakobo, ambaye alimpa jina la Israeli;

35 hao ambao Bwana alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, Msiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka;

36 ila yeye Bwana, aliyewaleta kutoka nchi ya Misri kwa nguvu nyingi, na kwa mkono ulionyoshwa, yeye ndiye mtakayemcha, yeye ndiye mtakayemsujudia, yeye ndiye mtakayemtolea sadaka;

37 na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.

38 Na hilo agano nililofanya nanyi, msilisahau; wala msiche miungu mingine;

39 lakini Bwana, Mungu wenu, ndiye mtakayemcha; naye atawaokoa mikononi mwa adui zenu wote.

Uhuru wa Mkristo;

Asubuhi hii tunasoma juu ya Agano kati ya Mungu na wana wa Yakobo (Israeli) kuhusu ibada, kuitii torati, na kutoabudu miungu. Bwana anawakumbusha kwamba ndiye aliyewatoa Misri utumwani, hivyo wasikilize maagizo yake na kutii sheria zake. Ukiendelea kusoma mbele kidogo unaona wakiendelea na ibada za sanamu;

2 Wafalme 17:40-41

40 Walakini hawakusikia, bali wakafanya sawasawa na kawaida zao za kwanza.

41 Basi mataifa hawa wakamcha Bwana, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; kama walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo.

Yesu Kristo aliyetuweka huru na dhambi kwa kutuokoa anatuita kumcha na kumtumikia yeye peke yake. Tutende yote kwa jina lake, kwa utukufu wake. Huo ndiyo wito kwetu, kuishi kwa kumcha Bwana siku zote za maisha yetu hata uzima wa milele. Amina

Siku njema

Heri Buberwa