
Jumamosi asubuhi tarehe 10.10.2026;
1 Wakorintho 9:16-23
16 Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!
17 Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili.
18 Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.
19 Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.
20 Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.
21 Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.
22 Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.
23 Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.
Uhuru wa Mkristo;
Mtume Paulo anaandika juu ya utume wake akisema ana ole asipoihubiri Injili, kazi ambayo aliifanya kwa hiari yake na kuiona thawabu. Paulo anasema kwa kuwa huru kwa watu wote alijifanya mtumwa wa wote ili apate watu wengi zaidi. Alikuwa Myahudi ili awape Wayahudi, pia alikuwa kama yuko chini ya sheria, ingawa hakuwa chini ya sheria.
Paulo anaongelea utume wake wa Injili, lakini akisema kwamba hakuwa chini ya sheria. Iko hivyo kwa wote tuliookolewa na Yesu Kristo, kwamba hatuko chini ya sheria. Tukumbushane kwamba kwa njia ya Yesu Kristo tuko huru na dhambi, siyo watumwa tena, hivyo tumwamini Kristo pekee. Amina
Siku mwema
Heri Buberwa
