VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Luka 7:1-10

Jumatano asubuhi tarehe 14.10.2026;

Luka 7:1-10

1 Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu.

2 Na mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana.

3 Aliposikia habari za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake.

4 Nao walipofika kwa Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili;

5 maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi.

6 Basi Yesu akaenda pamoja nao. Hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, yule akida alituma rafiki kwake, akamwambia, Bwana, usijisumbue, maana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu;

7 kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona.

8 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

9 Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii.

10 Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa ni mzima.

Imani yenye ushindi;
Akida mmoja alikuwa na mtumwa mgonjwa akamwendea Yesu akimuomba amponye mtumwa wake. Alikwenda na Yesu nyumbani kwake, akamuomba atamke neno tu maana aliona hastahili Yesu kuingia kwake. Aliwasimamia askari lakini alijiona hastahili Yesu kuingia kwake. Yesu akaiona imani yake akamponya mtumwa wake.
Yule akida aliona Yesu akitamka neno ingetosha tu, hii ilikuwa imani kubwa sana kama Yesu alivyosema kwamba alikuwa hajaona imani kama ile katika Israeli(10). Kwa imani ya yule akida mtumwa wake alipona. Kwa imani katika Yesu Kristo tunaweza kushinda yote. Amina

Siku njema

Heri Buberwa