VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Waebrania 11:8-12

Jumatatu asubuhi tarehe 12.10.2026;

Waebrania 11:8-12

8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.

9 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.

10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.

11 Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.

12 Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.

Imani yenye ushindi;
Somo la leo asubuhi linaonesha imani ya Ibrahimu na Sara walivyomwamini Mungu na kumtii hata bila kujua matokeo yake. Ibrahimu alihama nchi yake akaenda ugenini katika ile nchi ya ahadi. Sara alipokea uwezo wa kubeba mimba katika uzee kwa kuiamini ahadi ya Mungu, ukawa mwanzo wa vizazi kutoka kwa mtu mmoja.
Ibrahimu na Sara wanaonesha imani ya kweli katika Bwana, hawaishii kuwa na imani, bali wanakuwa watii kwa kuisikia na kuifuata sauti ya Mungu. Tunapoanza juma hili, tukumbushane kila mmoja wetu kusimama katika imani yetu kama tulivyoitwa. Imani ya kweli itatupa ushindi katika safari yetu ya imani na kuifikia mbingu tuliyoahidiwa na Bwana. Amina
Uwe na wiki njema ukiwa na imani yenye ushindi.

Heri Buberwa