1 Yohana 4:7-9 - 02-09-2026

Date
Reading
1 Yohana 4:7-9

Jumatano asubuhi 02.09.2026;

1 Yohana 4:7-9

7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.

8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.

9 Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.

Tumpende na kumjali jirani wetu;

Asubuhi ya leo tunamsoma Yohana katika waraka wake akiandika juu ya upendo. Yohana anaelekeza kupendana kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, amjua Mungu. Asiyependa hakumjua Mungu! Kwa maana Mungu ni upendo. 
Yohana anasema upendo wa Mungu ulionekana kwetu alipomtuma mwanae wa pekee kutukomboa. Kwa mfano huo tunaagizwa kupendana kama lilivyo agizo takatifu la Kristo aliye asili ya upendo. Mpende jirani yako kama nafsi yako. Amina

Siku njema

Heri Buberwa