DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 12 JULAI, 2026
SIKU YA BWANA YA 6 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI:
“UPENDO WA MUNGU NA UTAWALA”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni:Joseph Jackson kutoka Arusha.
3. Matoleo ya Tarehe 05/07/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
- Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 05/07/2026 ni Washarika 872 na Sunday School 254
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi na walezi kuwa mazoezi
Ya mikaeli na watoto yataanza Jumamosi ijayo tarehe 18/7/2026 muda watoto Wa kingereza ni saa 4:00 hadi saa 6:00 mchana, na watoto wa Kiswahili ni saa 8:00 hadi saa 9:30 alasiri.
8. Jumapili ijayo tarehe 19.07.2026 tutashiriki sakramenti ya meza ya Bwana Washarika tujiandae.
9. Jumapili ijayo tarehe 19.07.2026 katika ibada ya …Ndg. Fanaka John Eliafye wa Upanga Fire atamshukuru Mungu kwa ulinzi na kumtunza tangu baba yake alipo Twaliwa miaka 10 iliyopita.
Neno: Zaburi 103:1-6, wimbo namba 257 Jumapili ijayo tarehe 19.07.2026 katika ibada ya pili familia ya Prof. Fred Mhalu itatoa shukrani kwa ulinzi na faraja kwa kipindi cha Mwaka mmoja sasa tangu kutwaliwa kwa Prof Solomoni Mhalu.
Neno Zab 100:3-5 na wimbo Ee Mungu sikia kuomba kwangu kutoka kwaya ya Agape.
10. NDOA. Ndoa za washarika
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 01/08/2026
SAA 9.00 ALASIRI
Bw. Clinton Bariki Kiwelu na Bi. Sakshi Ghosh
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 18/07/2026
SAA 9.00 ALASIRI
Bw. Erick Richard Mtega na Bi. Dorina Nelson Zachwa
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: watasali hapa Kanisani saa moja kamili asubuhi.
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo Kwa Bw na Bibi Charles Lyimo.
- Kinondoni: kwa: Prof. Kulaba.
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa familia ya Bw na Bi Christopher Kivulenge.
- Oysterbay na Masaki: Kwa familia ya Chomba
12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azaniafront.or.tz, pia tupo Facebook na Instagram.
13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
