Date
Reading
Mithali 19:17
Jumamosi asubuhi tarehe 05.09.2026
Mithali 19:17
Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.
Tumpende na kumjali jirani wetu;
Jumamosi ya leo tunamsoma Suleimani akisema kuwa kumhurumia maskini ni kumkopesha Bwana, naye atamlipa kwa tendo jema. Hapa Suleimani anamaanisha kwamba kumhurumia maskini ni kumsaidia, na unapomsaidia ufahamu kwamba ni maskini hawezi kukulipa, mwenye kukulipa ni Bwana.
Kumhurumia maskini ni ujumbe unaotukumbusha kuwajali wasiojiweza kama familia na Kanisa kwa ujumla. Tunapokumbushana kuwapenda na kuwajali jirani zetu tuwakumbuke wasiojiweza pia. Maaskofu na Wachungaji zingatieni jambo hili la Diakonia, sina uhakika kama ni sahihi kuwa na bajeti kubwa ya TeHAMA kuliko Diakonia. Tuwapende na kuwajali jirani zetu, tusiwasahau wasiojiweza. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
