Date
Reading
Mithali 16:13
Alhamisi asubuhi 27.08.2026
Mithali 16:13
Midomo ya haki ni furaha ya wafalme; Nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa.
Tutumie ndimi zetu kwa Utukufu wa Mungu;
Leo asubuhi tunamsoma Mfalme Suleimani juu ya kusema kweli. Mfalme Suleimani anasema midomo ya haki ni furaha ya haki ya wafalme, yaani wafalme huwapenda raia watumiao midomo yao kuwasaidia wafalme. Anapomalizia "nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa" anamaanisha kuwa wafalme huwapenda raia wasemao kweli.
Bila shaka ukweli wa raia huwasaidia wafalme kupata taarifa sahihi ambazo huweza kuwa msaada kwa wafalme katika shughuli za kila siku katika utawala. Neno hili ni picha ya Yesu Kristo anayetutaka kusema kweli daima. Kama wafalme wa dunia hii wanaipenda kweli kutoka kwa raia, Yesu Kristo si zaidi? Tumia ulimi wako kwa Utukufu wa Mungu. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
