Date
Reading
Mithali 14:19
Ijumaa asubuhi terehe 24.07.2026
Mithali 14:19
Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki malangoni mwao wenye haki.
Neema ya Mungu yatosha;
Suleimani anaandika mithali ambazo ni mkusanyiko wa tofauti kati ya hekima na ujinga. Uko ushauri wa kila siku katika kazi, maongezi, maamuzi, mahusiano n.k Mstari wa leo asubuhi kama somo ni wabaya kuinama mbele wa wema na wasio haki mlangoni mwao wenye haki.
Ni mstari unaotukumbusha kwamba mafanikio ya uovu ni ya muda, bali Kristo hudumu daima. Wenye haki wanaweza wasipate haki yao kwa wakati, lakini upo wakati ambao na wao watafurahi kwa neema ya Mungu. Kumbe tuvumilie katika maisha yetu maana Yesu hachelewi, na hatuachi. Neema yake yatosha. Amina.
Siku njema
Heri Buberwa
