VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
1 Wakorintho 6:12-13

Jumanne asubuhi tarehe 06.10.2026;

1 Wakorintho 6:12-13

12 Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.

13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.

Uhuru wa Mkristo;

Mtume Paulo anaandika kwamba vitu vyote ni halali kwake, lakini si vyote vifaavyo, na hawezi kutiwa chini ya uwezo wa kitu chochote. Paulo anaendelea kusema vyakula ni tumbo na tumbo kwa vyakula, lakini vyote vina mwisho wake. Paulo anamalizia kwa kusema mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.
Ujumbe wa Paulo ni kumtukuza Mungu katika mwili na roho katika maisha yetu kwa sababu tuko huru kwa njia ya wokovu. Tusitumie nafasi zetu vibaya, pasipo utukufu wa Mungu, wala mali/nafasi zetu zisitutenge na Mungu. Katika yote tufanyayo, tuzingatie sifa kwenda kwa Mwenyezi Mungu atuwekaye huru na dhambi. Amina

Siku njema

Heri Buberwa