Zekaria 8:16-17 - 31-08-2026

Date
Reading
Zekaria 8:16-17

Jumatatu asubuhi 31.08.2026;

Zekaria 8:16-17

16 Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme kweli na jirani yake; hukumuni kweli na hukumu ya amani malangoni mwenu;

17 wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema Bwana.

Tumpende na kumjali jirani wetu;

Tunaanza juma kwa kusoma ujumbe wa Mungu akiwataka watu kusema kweli na jirani, kwa amani na nia njema. Mungu kupitia kwa Nabii Zekaria anaendelea kuwataka watu wake wasiwaziane mabaya kama majirani, wasiape uongo, maana hayo ni machukizo kwa Bwana. 

Tunaanza juma kwa kujifunza nini?

1. Ongea ukweli - Epuka kusema uongo maana hiyo ni dhambi

2. Tenda haki - Mpe kila mmoja haki yake kwa nafasi yako hapo ulipo

3. Tenda wema - Tenda wema kwa jirani zako. Acha kuishi kwa kuvuruga watu

4. Usiape kwa uongo - Usitumie uongo kuumiza wengine, unaweza kufurahi kwa kuumiza wengine ukafanikiwa. Lakini furaha yako ni ya muda tu maana utawajika mbele za Mungu.

5. Mpende jirani yako kama nafsi yako. Amina

Uwe na wiki njema ukimpenda jirani yako

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com