Date
Reading
Zekaria 11:15-17

Jumanne asubuhi tarehe 20.10.2026;
Zekaria 11:15-17
[15]BWANA akaniambia, Jitwalie tena vyombo vya mchungaji mpumbavu.
[16]Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuzirarua-rarua kwato zao.
[17]Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kuume; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kuume litakuwa limepofuka.
Madhara ya kudharau wito;
Nabii Zekaria katika sura ya 11 anatoa utabiri akiwaonya wachungaji wasiotimiza wajibu wao. Kwenye mstari wa 15 tunaona kuna hadi Mchungaji mpumbavu! Mstari wa mwisho (17) unahitimisha kwa kutoa onyo kwake Mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi. Bwana anasema upanga utakuwa juu yake! Mkono wake utakuwa umekauka, na jicho lake la kuume litakuwa limepofuka!
Asubuhi hii tunaitwa kuwa wema kama alivyo Kristo Yesu, ili tuiepuke hasira ya Mungu. Ni kwa kutimiza wajibu wetu tukifanya yatupasayo, hasa kumtangaza Kristo aliye Mchungaji mwema, ili wote waokolewe katika yeye. Tutimize wajibu wetu katika utume wetu maana tutatoa hesabu. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
