VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Yoshua 22:13-20

Ijumaa asubuhitarehe  23.10.2026;

Yoshua 22:13-20

13 Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, hata nchi ya Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani;

14 na pamoja naye wakuu kumi, mkuu mmoja wa nyumba ya mababa kwa ajili ya kila kabila ya Israeli; nao kila mmoja alikuwa ni kichwa cha nyumba ya mababa katika maelfu ya Israeli.

15 Nao wakawafikilia hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakasema nao, wakinena,

16 Mkutano wote wa Bwana wanena, Ni kosa gani hili mlilolikosa juu ya Mungu wa Israeli, hata mkakengeuka hivi leo na kuacha kumwandama Bwana, katika kujijengea madhabahu, na kuasi hivi leo juu ya Bwana?

17 Je! Ule uovu wa Peori haututoshi, ambao hamjajitakasa nafsi zenu katika huo hata hivi leo, ijapokuwa ilikuja tauni juu ya mkutano wa Bwana,

18 hata ikawa hamna budi hivi leo kugeuka na kuacha kumwandama Bwana? Kisha itakuwa, kwa kuwa ninyi mwamwasi Bwana hivi leo, kwamba kesho yeye atakasirika na mkutano wote wa Israeli.

19 Basi kwamba hiyo nchi ya milki yenu si tohara, ndipo ninyi vukeni na kuingia nchi ya milki yake Bwana, ambayo maskani ya Bwana inakaa ndani yake, nanyi twaeni milki kati yetu; lakini msimwasi Bwana, wala msituasi sisi, kwa kujijengea madhabahu zaidi ya hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wetu.

20 Je! Huyo Akani mwana wa Zera hakukosa katika vile vitu vilivyowekwa wakfu, na hasira ikauangukia mkutano wote wa Israeli? Kisha mtu huyo hakuangamia peke yake katika uovu wake?

Madhara ya kudharau wito;
Katika somo la asubuhi ya leo, Finehasi na viongozi wa makabila kumi waliwakabili makabila ya mashariki ya Gadi na Rubeni, na nusu ya kabila la Manase katika Gileadi, wakiwatuhumu kuasi kwa kujenga madhabahu isiyo halali. Waliwaambia kwamba uasi kwa Mungu ungeleta hasira ya Mungu kwa Israeli hapo baadaye. 
Katika safari ya imani tunao wajibu wa kuhakikisha maisha yetu yanaakisi utukufu wa Mungu. Yaani tusifanye yaliyo mapenzi yetu, bali yaliyo mapenzi ya Mungu. Huo ndiyo wito wetu, kumfuata Yesu Kristo aliye Mwokozi wetu. Amina

Siku njema

Heri Buberwa