Warumi 13:1-7 - 08-09-2026

Date
Reading
Warumi 13:1-7

Jumanne asubuhi tarehe 08.09.2026;

Warumi 13:1-7
1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.
3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;
4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.
5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri.
6 Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo.
7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.

Tutende wajibu wetu kwa Mungu kwa uaminifu;

Asubuhi ya leo tunasoma juu ya kuitii mamlaka. Paulo anawaandikia watu wa Rumi kuitii mamlaka iliyo kuu maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu. Paulo anasema amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu. Mkazo wa Paulo ni kuwa wenye mamlaka ni watumishi wa Mungu kwa watu, hivyo waheshimiwe. Kwa hiyo kuwatii ni lazima maana huo ni wajibu.

Paulo anatukumbusha wajibu wetu kama kundi la waaminio, kila mmoja kumheshimu mwenzake na kumuona bora, lakini kubwa zaidi kuitii mamlaka "halali". Kuwa mtii kwa mamlaka kunaendana na unyenyekevu, na kutimiza wajibu wako hapo ulipo, yaani kuwajibika kwa nafasi yako. Kumbe somo linatukumbusha uwajibikaji, yaani uwakili mwema mbele za Mungu maana tutatoa hesabu ya uwakili wetu. Amina
Siku njema

Heri Buberwa