Warumi 12:6-8 - 07-09-2026

Date
Reading
Warumi 12:6-8

Jumatatu asubuhi tarehe 07.09.2026;

Warumi 12:6-8

6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;

7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;

8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.

Tutende wajibu wetu kwa Mungu kwa uaminifu;
Mtume Paulo analiita Kanisa la Rumi kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu kwa umoja wao. Mistari tuliyoisoma ni maelekezo kwa kila mmoja kutumia karama yake kwa kadri ya neema aliyopewa ikiwa unabii, huduma, kufundisha, kuonya, kukirimu. Na mimi naongezea, kuhubiri, kuimba, diakonia, uinjilisti, mzee wa Kanisa, mkurugenzi wa ofisi, mwalimu, askari n.k
Ni wito wangu kwako kutimiza wajibu wako hapo ulipo. Kazi unayoifanya ni utume kamili mbele za Mungu (iwe ni kazi halali) maana Mungu amekupa kazi hiyo na anakupa nguvu ili uendelee kumtumikia kwa njia hiyo. Basi tenda kazi yako kwa uaminifu maana huo ndiyo uwakili mwema mbele za Mungu. Amina

Uwe na wiki njema yenye uwajibikaji 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com