VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Ufunuo wa Yohana 19:11-16

Jumatatu asubuhi tarehe 16.11.2026;

Ufunuo wa Yohana 19:11-16

11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.

Hukumu ya mwisho inakuja;
Yohana aliona mbingu zimefunuka na farasi mweupe, na aliyempanda anaitwa "Mwaminifu na Wa-kweli", anayehukumu na kupiga kwa haki. Macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, juu ya kichwa chake kulikuwa na vilemba vingi (taji nyingi), na ana jina lililoandikwa ambalo hakuna anayelijua ila yeye mwenyewe. Alikuwa amevaa vazi lililochovywa katika damu na jina lake anaitwa "Neno la Mungu".
Majeshi yaliyo mbinguni yalimfuata yakiwa yamepanda farasi weupe na wamevaa kitani nzuri, nyeupe na safi. Upanga mkali hutoka kinywani mwake ili kuwapiga mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma na kukanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. Ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake: MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA
Tunapoanza juma kwa kutafakari hukumu ya mwisho, somo linatufundisha kuhusu kuja kwa mara ya pili kwa Yesu Kristo duniani kwa utukufu mkubwa, si kama mtumishi au Mwana-Kondoo wa upole, bali kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwaba ili kuleta hukumu ya haki na kukomesha uovu.
Mambo makuu yanayofundishwa katika somo la asubuhi ya leo;
1. Yesu Kristo ndiye mwaminifu na wa-kweli (11). Anarudi kutimiza ahadi zake za kuwaokoa walio wake na kuhukumu ulimwengu kwa uadilifu. Farasi mweupe anawakilisha ushindi na utakatifu.
2. Mamlaka na hukumu ya Kristo (12-13)
- Macho yake kama mwali wa moto yanaashiria uwezo wake wa kupenya na kuona kila kitu kwa haki
- Vilemba vingi kichwani vinamaanisha umiliki na ukuu wake juu ya falme zote
- Vazi lililochovywa katika damu linaashiria ushindi wake kupitia dhabihu yake na mapambano dhidi ya uasi
- Anaitwa "Neno la Mungu" ikithibitisha uungu wake na utimilifu wa neno la Mungu 
3. Ushiriki wa majeshi ya mbinguni (14) - Anashuka akiwa ameandamana na majeshi ya mbinguni (watakatifu na malaika) waliovaa mavazi meupe na safi wakiwa wamepanda farasi weupe kuonesha ushindi wa mwisho wa haki
4. Nguvu ya neno lake (15). Upanga mkali utokao kinywani mwake unaonesha kuwa anashinda mataifa kwa Neno lake na kuleta utawala wa fimbo ya chuma (hukumu isiyopingika)
5. Utambulisho wake wa kilele (16). Ameandikwa jina wazi kwenye vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA" kuonesha kuwa enzi na mamlaka yote ni yake milele.
Muktadha wa somo ni ujio wa Kristo kwa mara ya pili kulichukua Kanisa, ambapo atakuja kwa utukufu kuhukumu ulimwengu. Hukumu yake ni ya haki. Jiandae kwa mwisho huo. Amina
Uwe na wiki njema ukikumbuka kwamba  hukumu ya mwisho ipo.

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com