Date
Reading
Mithali 1:28-33

Jumamosi asubuhi tarehe 24.10.2026;
Mithali 1:28-33
28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
29 Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha Bwana.
30 Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote.
31 Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe.
32 Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.
33 Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.
Madhara ya kudharau wito;
Somo linahusu hekima ya Mungu. Linaeleza madhara ya kuikosa au kuiacha hekima ya Mungu. Waiachao hekima ya Mungu watamuita Bwana hataitika, watamtafuta kwa bidii wasimuone. Watakula matunda ya kuikataa hekima ya Mungu.
Hekima ya Mungu hutuongoza kuwaza, kunena na kutenda kwa usahihi. Yaani hekima ya Mungu hutuongoza kutenda yaliyo mapenzi ya Mungu. Yesu anapotuita, anatutaka kutenda yaliyo mapenzi yake, ambayo hatuwezi kuyatimiza pasipo hekima itokayo kwake. Tuombe hekima ya Kristo isiondoke kwetu ili tudumu katika wito wa kumtumikia kama alivyotuita. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
