%AutoEntityLabel: 7cf519b8-cd81-482b-9868-5b52bf3f548c%

Date
Reading
Mathayo15:21-28

Ijumaa asubuhi tarehe 21.08.2026;

Mathayo 15:21-28

21 Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.

22 Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.

23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.

24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.

26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.

28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

Mungu huwainua wanyenyekevu;

Somo la leo asubuhi ni sawa na lililokuwa somo la mahubiri la Jumapili iliyopita (lilitoka Injili ya Marko). Mwanamke Mkananayo alimjia Yesu akiomba uponyaji kwa binti yake aliyekuwa na pepo mchafu. Injili ya Mathayo inaeleza vizuri, pale Yesu anaposema alikuja kwa ajili ya kondoo waliopotea kwa Israeli (yule mama hakuwa Myahudi)

Pamoja na Yesu kumwambia yule mama kwamba si vema kuwapa mbwa chakula cha watoto, yule mwanamke alisema hata mbwa hula makombo chini ya meza. Mwanamke alionesha imani na unyenyekevu kwa Yesu, binti yake akaponywa. Tunakumbushwa kuwa wenye imani na unyenyekevu. Amina

Siku njema

Heri Buberwa