VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
Mathayo 5:4-8

Jumatano asubuhi tarehe 04.11.2026;

Mathayo 5:4-8

4 Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.

5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.

6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.

7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.

8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.

Tunaitwa kuwa wenyeji wa Mbinguni;
Ni sehemu ya hotuba ya Yesu mlimani kuhusu yapasayo katika Ufalme wa Mungu. 
- Wenye huzuni - Inahusu wale wenye kuhuzunika kila wakati kwa sababu ya dhambi zao na maumivu wanayopitia katika njia ya imani. Hawa wanaahidiwa faraja.
- Wenye upole - upole siyo udhaifu, bali ni nguvu itufanyayo kumtegemea Mungu, na siyo nguvu zetu. Wenye upole hawagombani. Hawa ahadi yao ni kuirithi nchi.
- Wenye njaa na kiu ya haki - hawa ni wale wenye haja ya kumtafuta Mungu na uwezo wake, sawa na mtu atafutaye chakula. Mungu anaahidi kuwashibisha.
- Wenye rehema - hawa wana huruma, msamaha, wema kwa wengine n.k wanaahidiwa rehema vilevile.
- Wenye moyo safi - wasifu usio na hila wala unafiki, kumtafuta Mungu na kuishi maisha yampendezayo. Wanaahidiwa kumuona Mungu.
Hizo "Heri" ni baadhi tu, zikionesha kwamba yafaa kuwaza, kunena na kutenda apendavyo Mungu ili kuingia katika ufalme wake. Na tumche Bwana kama atakavyo ili tuwe wenyeji wa Mbinguni. Amina

Siku njema

Heri Buberwa