DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 06 SEPTEMBA, 2026 SIKU YA BWANA YA 14 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI:
“TUTENDE WAJIBU WETU KWA MUNGU KWA UAMINIFU”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni:Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 30/08/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
- Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 30/08/2026 ni Washarika 747 na Sunday School 238
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi na walezi kuwa mazoezi Ya mikaeli na watoto yanaendelea kila Jumamosi. Muda, kwa ibada ya kingereza ni saa 3:00 hadi saa 6:00 mchana, na ibada ya Kiswahili ni saa 6:00 hadi saa 8:00 mchana.
8. Kutakuwa na Ibada maalum ya Wajane na Wagane Kijimbo itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 20.09.2026 kuanzia saa 8:00 mchana katika Usharika wa Kipawa.Ibada hii itaongozwa na Mkuu wa Jimbo na itaambatana na Sakramenti ya meza ya Bwana.
9. Kwaya ya Umoja inaendelea na mazoezi ya Reformation kila Jumanne na Jumatano saa 11:00 jioni. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kwa wakati.
10. Vitabu vya Ibada ya nyumba kwa nyumba vinapatikana dukani.
11. Jumapili ijayo ya tarehe 13.09.2026 tutatoa sadaka ya Msamaria Mwema. Sadaka hii ni kwa ajili ya kusaidia vituo vyetu vya Diakonia.
12. Shukrani
Leo katika ibada zote tatu Viongozi wa Umoja wa Wanawake watatoa sadaka ya shukrani kwa wito wa kuliongoza kundi la Umoja wa Wanawake,Wanamwomba Mungu awaongoze ili wawe na Ushirikiano na kufanyika Baraka kwa Kanisa lake. Wanaomba wanawake wote waungane nao katika shukrani hii.
Neno Zab 92:1 na wimbo namba 390 (Bwana asema nimtume nani)
13. NDOA. Ndoa za Washarika; Hakuna ndoa ya Msharika.
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
14. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Itafanyika Kanisani siku ya Jumamosi saa 1:00 kamili asubuhi.
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo kwa Mama Mamkwe.
- Kinondoni: kwa: Prof. G. Mmari
Tegeta,Kunduchi,BahariBeach,Ununio,Boko:Kwa Bw&Bibi Nyamagege Buchanagandi
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bibi James Monyo
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: kwa Robinson Monyo
- Upanga: Kwa Bi Frida Ndossi
15. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya azaniafront.or.tz; pia tuna kurasa Facebook na Instagram.
16. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
