DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO
YA USHARIKA TAREHE 30 AGOSTI, 2026 SIKU YA BWANA YA 13 BAADA YA UTATU NENO LINALOTUONGOZA NI:
“TUMPENDE NA KUMJALI JIRANI WETU”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni:Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 23/08/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
- Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 23/08/2026 ni Washarika 845 na Sunday School 220
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi na walezi kuwa mazoezi Ya mikaeli na watoto yanaendelea kila Jumamosi. Muda, kwa ibada ya kingereza ni saa 3:00 hadi saa 6:00 mchana, na ibada ya Kiswahili ni saa 6:00 hadi saa 8:00 mchana. Aidha, T-shirt za mikaeli na watoto zinapatikana dukani.
8. Kwaya ya Umoja inaendelea na mazoezi ya Reformation kila Jumanne na Jumatano saa 11:00 jioni. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kwa wakati.
9. Vitabu vya Ibada ya nyumba kwa nyumba vinapatikana dukani.
10. Kutakuwa na mkesha wa wanawake kijimbo utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 04/09/2026 katika Usharika wa Kariakoo kuanzia saa 3:00 usiku.
11. Shukrani
- Leo katika ibada ya tatu Christina Paul Kiboma atamtolea Mungu sadaka ya shukrani kwa kumponya Christina baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa Scitical pain, Pia Binti yake Dr. Chrisha Imani kwa kumbukizi ya kuzaliwa tarehe 28.08.2018
Neno Yer 33:3 na wimbo namba 257 Haya ee moyo wangu
- Leo katika ibada ya tatu Familia ya marehemu Mchungaji Christian Mushumbusi itamtolea Mungu shukrani ya pekee kwa kuwa pamoja nao kwa kipindi chote cha msiba wa mama yao mpendwa Edith Mushumbusi na kufanikisha mazishi yake nyumbani kwao Kibeta Bukoba.
Neno Ufunuo 3:5-6 na wimbo namba 305, na Kwaya Kuu Vita vya nchi Yesu kashinda
- Jumapili ijayo ya tarehe 06/09/2026 katika ibada zote tatu Viongozi wa Umoja wa Wanawake watatoa sadaka ya shukrani kwa wito wa kuliongoza kundi la Umoja wa Wanawake,Wanamwomba Mungu awaongoze ili wawe na Ushirikiano na kufanyika Baraka kwa Kanisa lake. Wanaomba wanawake wote waungane nao katika shukrani hii.
Neno Zab 92:1 na wimbo namba 390 (Bwana asema nimtume nani)
12. NDOA. Ndoa za Washarika
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 04.09.2026
SAA 8:00 MCHANA
Bw.Issaya Y. Igosi na Bi Johary T. Kilagwa
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Itafanyika Kanisani siku ya Jumamosi saa 1:00 kamili asubuhi.
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo Kwa Dr. & Bibi Jimmy Mbelwa
- Kinondoni: kwa: Dr. & Bibi Onesmo
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach,Ununio,Boko: Kwa Bw & Bibi Frank Korassa
- Oysterbay na Masaki: Kwa Mama Nisile Mollel
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: kwa Vicky Mandari
- Madale, Goba, Mivumoni: kwa Bw & Bibi Shadrack Kombe
14. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya azaniafront.or.tz, pia tuna kurasa Facebook na Instagram.
15. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
