VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 18 OKTOBA 2026, SIKU YA BWANA YA 20 BAADA YA UTATU.

NENO LINALOTUONGOZA  NI:

  “ MADHARA YA KUDHARAU WITO’’

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 11/10/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

- Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe  11/10/2026 ni Washarika  704  na Sunday School  223

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=

7. Kwaya ya Umoja watashiriki Uimbaji ngazi ya  Dayosisi awamu ya kwanza  leo katika Usharika wa Yombo. Tuwaombee.

8. Kwaya ya Agape wanawashukuru sana washarika wote waliojitoa na wanaendelea kuungana nao katika kupata pikipiki 10 zitakazoenda Missioni ya Tabora Mungu awabariki. Mpaka sasa zimepatikana pikipiki 5 wanaendelea kuwaomba Washarika kuungana nao ili kufikia lengo. Changia kupitia Akaunti 013874006021 Agape Azania Front au fika Ofisi ya Usharika kwa Mhasibu au ukamuona kiongozi wa Kwaya ya Agape.

9. Uongozi wa Umoja wa Wanawake Azania Front Unapenda kuwatangazia Washarika wanawake wote kuwa tunaendelea kujiandikisha katika Umoja wa Wanawake (UWA) kupitia fomu Maalum. Dhumuni la kujiandikisha ni ili kuwatambua na kushirikiana kwa pamoja kufanya majukumu yetu katika Kanisa,Kujengana Kiroho na kudumisha Upendo na Amani kwa Wanawake wote na Usharika kwa Ujumla. Tunaomba kila mwanamke ajaze fomu na kurudisha leo leo.

10. Kamati ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kuwatangazia kuwa semina ya Elimu ya Afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa mwaka huu itafanyika Jumamosi tarehe 21.11.2026 saa 2:00 Asubuhi hadi saa 9;00 Alasiri. Mafunzo haya ni kwa wanafunzi wa Kipaimara wa mwaka wa kwanza na wa pili pamoja na wale waliohitimu miaka ya karibuni wenye umri chini ya miaka 15,  Aidha, semina hii pia itakuwa kwa wazazi na walezi wa wanafunzi hao.

11. Leo  ni Sikukuu ya mavuno. Washarika tunakaribishwa kumtolea Mungu mavuno kwa moyo wa kupenda.

12. SHUKRANI

 Mama Aida  Mwakisu atamtolea Mungu sadaka ya shukrani Jumapili ijayo tarehe  25.10.2026 katika ibada ya tatu Kwa kutimiza miaka 70 ya kuzaliwa.

 Neno Zaburi 138:1-5 na wimbo kutoka Kwaya Kuu  ( Ee Mungu wangu uliye Mbinguni   mwanao nakuja kushukuru)

13. NDOA. Ndoa za Washarika

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 07.11.2026

  • Kati ya Bw. Benson Peter Katanga na Bi. Lightness Samwel Mbise
  • Bw. Issack Godfrey Kapaga na Bi. Flora Juma Petro
  • Bw. Erick A. Mbwambo na Bi. Naomi B. Masanja

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 01.11.2026

SAA 9:00 ALASIRI

  • Kati ya Bw. Arnold Charles Mkony na Bi. Dorothea Erasmus Mbosha

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

14. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Mjini kati: Itafanyika Kanisani siku ya Jumamosi saa 1:00 kamili asubuhi.
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo Kwa Bw. & Bibi Kenneth Zebedayo  
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: kwa Familia ya Filex Mosha
  • Upanga: Kwa Bw. & Bibi  George  Kinyaha
  • Madale, Goba, Mivumoni: kwa..

15. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya azaniafront.Or.tz, pia tupo Facebook na Instagram.

16. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.

 Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki