Matangazo ya usharika Tarehe 2 Agosti 2026

DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI MATANGAZO  YA USHARIKA  TAREHE  02 AGOSTI, 2026

SIKU YA BWANA YA 9 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA  NI:

MWENENDO WENU UWE WA HEKIMA”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:hakuna mgeni aliyetufikia na cheti: Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.

3. Matoleo ya Tarehe 26/07/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 19/07/2026 ni Washarika 802 na Sunday School  219

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili. Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi na walezi kuwa mazoezi Ya mikaeli na watoto yanaendelea kila Jumamosi.  Muda, kwa ibada ya kingereza ni saa 3:00 hadi saa 6:00 mchana, na ibada ya Kiswahili ni saa 6:00 hadi saa 8:00 mchana.

8. Kwaya ya Umoja inaendelea na mazoezi ya Reformation kila Jumanne na Jumatano  saa 11:00 jioni. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kwa wakati.

9. Leo  tarehe 02.08.2026 katika ibada ya tatu kutakuwa na tendo la kuwabariki wazee wa Kanisa na kuwaingiza  kazini. Aidha leo tutashiriki sakrament ya meza ya Bwana katika ibada zote, Washarika tunakaribishwa.

10. Jumapili ijayo tarehe 09.08.2026 katika ibada ya kwanza na ya tatu kutakuwa na tendo la kuwaingiza Viongozi wa vikundi pamoja na viongozi wa Jumuiya kazini, Viongozi wote mnaombwa kuwepo.

11. Vitabu vya nyumba kwa nyumba vinapatikana duka letu la vitabu.

12. Kutakuwa na Afya check itakayofanyika Jumamosi tarehe 22-08-2026 hapa Kanisani kuanzia saa 3:00 hadi saa 9:00 alasiri. Kutakuwa na station 12 ambazo zitakuwa na wataalam mbalimbali wa Afya ili kutoa huduma za kupima afya. Huduma zitakazotolewa ikiwemo: Macho, moyo,uchunguzi na ushauri wa cancer n.k pia tunakaribisha watu kutoa damu kwa ajili ya wahitaji mahospitalini.

13. Baraka ya Mtoto

  • Familia ya Bw. na Bibi Joseph Elihudi Kivulenge wamejaliwa mtoto wa kike tarehe

29.07/2026. Baba,mama na mtoto wanaendelea vizuri.  

14. Shukrani

Jumapili ijayo tarehe 09.08.2026 katika ibada ya tatu Suzana Greyson Kuserwa atatoa shukrani kwa Mungu kwa matendo makuu aliyomfanyia.

Neno Zab 124:1-4 na wimbo n am b a 2 9 5( Mungu amenihurumia).

15. NDOA. Ndoa za Washarika Hatuna ndoa ya Msharika  

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

16. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mjini kati: Watasali hapa Kanisani saa moja asubuhi

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo

Kwa Bw & Bibi Charles Lyimo

- Kinondoni: kwa: Danford Mariki

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: kwa Victor Kida

- Upanga: Kwa Bw. & Bibi Zimba

- Madale, Goba, Mivumoni: kwa Bw & Bibi Shadrack Kombe.

17. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya azaniafront.or.tz, pia tupo Facebook na Instagram.

18. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.