DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 19 JULAI, 2026
SIKU YA BWANA YA 7 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI:
“NEEMA YA MUNGU YATOSHA”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni:hakuna mgeni aliyetufikia na cheti: Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.
3. Matoleo ya Tarehe 12/07/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
- Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONTCATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 1 2 /07/2026 ni Washarika 728 na Sunday School 204
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral Tv
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi na walezi kuwa mazoezi Ya mikaeli na watoto yanaendelea kila Jumamosi. Muda, kwa ibada ya kingereza ni saa 3:00 hadi saa 6:00 mchana, na ibada ya Kiswahili ni saa 6:00 hadi saa 8:00 mchana.
8. Kwaya ya Umoja itaendelea na mazoezi ya Reformation Jumanne tarehe 21.07.2026 saa 11:00 jioni. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kwa wakati.
9. Leo tarehe 19.07.2026 katika ibada zote tutashiriki sakramenti ya meza ya Bwana Washarika tunakaribishwa.
10. Jumapili ijayo tarehe 26.07.2026 katika ibada ya tatu Familia ya Elisha Mushumbusi itamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na Bwana Elisha Mushumbusi kustaafu kwa amani na furaha,Watoto wao (Moureen kupata mtoto, Edith kumaliza masomo yake ya Degree ya pili huko Marekani, kurudi nyumbani salama na kupata kazi, Baraka kumaliza kidato cha nne anajiandaa kwenda kidato cha tano.
Neno: Zaburi 9:1-2, Na wimbo Mungu kanilinda mimi kutoka Kwaya Kuu.
Jumapili ijayo tarehe 26.07.2026 katika ibada ya tatu Bibi Anna Mathias Kavugha atatoa shukrani kwa Mungu kwa ulinzi wa ajali na magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumbukizi ya miaka 90 ya kuzaliwa.
Neno Zab 103:1-5 na wimbo Huniongoza Mwokozi kutoka kwaya Kuu.
Jumapili ijayo tarehe 26.07.2026 katika ibada ya pili familia ya Dr.Mwambona/Chambo itamshukuru Mungu kwa mema mengi aliyowatendea katika Maisha yao.
Neno zaburi 9:1 na wimbo Amazing Grace, my chains are gone by New Chapter Choir
11. NDOA. Ndoa za washarika
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 01/08/2026
SAA 9.00 ALASIRI
- Bw. Clinton Bariki Kiwelu na Bi. Sakshi Ghosh
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: kwa Linda Felician
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo
Kwa Bw & Bibi Charles Lyimo
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Familia ya Bi Elyfrida Njowoka.
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bw & Bibi Itemba - Oysterbay na Masaki: Kwa Bw & Bibi Geofrey Mchangila
- Upanga: Kwa Bw &Bibi Mathias Kavugha
13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azaniafront.or.tz, pia tupo Facebook na Instagram.
14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
