Luka 6:27-29 - 03-09-2026

Date
Reading
Luka 6:27-29

Alhamisi asubuhi tarehe 03.09.2026;

Luka 6:27-29

27 Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,

28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.

29 Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.

Tumpende na kumjali jirani yetu;

Injili ya Luka huiandika hotuba ya Yesu mlimani kwa ufupi. Somo la asubuhi ya leo ni sehemu ya hotuba hiyo ambapo Yesu anafundisha juu ya upendo kwa adui. Anafundisha umati kuwapenda adui na kuwatendea mema wanaowachukia. Anaendelea kufundisha kuwabariki wanaowalaani na kuwaombea wanaowaudhi. Msitari wa 29 unafundisha kutolipiza kisasi.
Fundisho la upendo kwa jirani zetu linaendelea. 
Unampenda adui yako?
Unawatendea mema wanaokuudhi?
Unawabariki wanaokulaani?
Unawaombea wanaokuonea?
Haulipizi kisasi?
Zingatia upendo kwa jirani zako, maana hiyo ndiyo amri kuu. Amina

Siku njema

Heri Buberwa