Date
Reading
Luka 6:20-23

Ijumaa asubuhi tarehe 06.11.2026;
Luka 6:20-23
20 Akainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, Heri ninyi mlio maskini, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu.
21 Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka.
22 Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
23 Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.
Tunaitwa kuwa wenyeji wa Mbinguni;
Luka anaiandika hotuba ya Yesu mlimani kwa ufupi. Somo tulilosoma ni sehemu hiyo ya hotuba ya mlimani katika Injili ya Luka. Yesu anawatia moyo waliomsikiliza kwamba heri walio maskini, maana ufalme wa Mungu ni wao. Anawatia moyo wenye njaa kwamba watashiba, wanaochukiwa anawatia moyo kwamba wafurahi maana thawabu yao ni kubwa mbinguni.
Kama tulivyoona Jumatano ya juzi asubuhi, Yesu alikuwa anafundisha umuhimu wa kuwaza, kunena na kutenda kama atakavyo yeye, yaani kwa utukufu wake ili kuingia katika ufalme wake. Na tumche yeye na kutenda atakavyo ili tuwe wenyeji wa Mbinguni. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
