Luka 15:8-10 - 01-08-2026

Date
Reading
Luka 15:8-10

Jumamosi asubuhi tarehe 01.08.2026;

Luka 15:8-10

8 Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?

9 Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.

10 Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.

Mungu hupendezwa na moyo wa toba;

Sura ya 15 ya Injili ya Luka inafundisha juu ya huruma ya Mungu kwa mifano ambayo inaonesha kuacha wengi na kutafuta mmoja aliyepotea. Katika sura hii Luka anaandika mafundisho ya Yesu kuhusu;

1. Mfano wa kondoo aliyepotea (1-7)

2. Mfano wa sarafu iliyopotea (8-10)

3. Mfano wa mwana mpotevu na kaka yake (11-32)

Somo la asubuhi hii ni sehemu ya pili inayohusu sarafu iliyopotea, kwa mfano wa mwanamke mwenye shilingi kumi ambaye akipotewa na moja huacha kazi nyingine na kuitafuta hadi aipate. Akiipata huwa ni furaha! Ni mfano wa Mungu apendavyo watu wake watubu, na kuwapokea kwa upendo pale wanapotubu. Tumrudie Bwana kwa toba, maana yeye hupendezwa na moyo wa toba. Amina

Siku njema.

Heri Buberwa