Date
Reading
Luka 10:38-42
Alhamisi asubuhi tarehe 06.08.2026
Luka 10:38-42
38 Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake.
39 Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.
40 Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie.
41 Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;
42 lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.
Mwenendo wenu uwe wa hekima;
Yesu aliingia nyumbani kwa Martha aliyekuwa na ndugu yake aliyeitwa Mariamu. Martha akawa anaendelea na taratibu za kumkaribisha Yesu pale nyumbani, wakati huo Mariamu akaketi kumsikiliza Yesu akinena. Martha akalalamika kwa Yesu kwamba Mariamu hakumsaidia kazi pale nyumbani, amwambie amsaidie.
Yesu akamwambia Martha kwamba alisumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi, wakati Martha alichagua fungu jema. Tutimize wajibu wetu, lakini huo wajibu usitutoe kwa Kristo. Hiyo ndiyo hekima ifaayo, kutenda yote kwa kumtanguliza Bwana. Amina.
Siku njema
Heri Buberwa
