Date
Reading
Isaya 50:4
Ijumaa asubuhi tarehe 28.08.2026
Isaya 50:4
Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.
Tutumie ndimi zetu kwa Utukufu wa Mungu;
Nabii Isaya anasema Mungu amempa ulimi wa hao wafundishwao ili apate jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka. Baadhi ya wasomi wa Agano la kale huuona mstari huu kama unamtaja Yesu Kristo ambaye alitoka kwa Baba akafanya kazi kwa kumsikiliza ili kuuokoa ulimwengu (yaani Yesu akafanya kazi kwa kumsikiliza Baba).
Isaya anaposema Mungu amempa ulimi, anamaanisha kwamba matumizi yake ya ulimi katika kutangaza ujumbe wa Bwana ni kwa msaada wa Mungu. Ndiyo mfano wa Kristo Yesu aliyeifanya kazi yake kwa msaada wa Baba yake. Tunaweza kuzitumia ndimi zetu kwa Utukufu wa Mungu, kwa msaada wa Mungu mwenyewe. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
