1 Yohana 3:10-12 - 04-09-2026

Date
Reading
1 Yohana 3:10-12

Ijumaa asubuhi tarehe 04.09.2026;

1 Yohana 3:10-12

10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi;

12 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

Tumpende na kumjali jirani wetu;

Bwana Asifiwe;
Leo asubuhi tunamsoma Yohana akisema watoto wa Mungu hutenda haki na kupendana. Anaendelea kusema kwamba fundisho la kupendana liko tangu kale. Anamrejea Kaini alivyomuua ndugu yake (Mwz 4:1-16) kwamba huo ulikuwa uovu. 
Sisi kama wakristo tuliookolewa ni wana wa Mungu, basi kama Yakobo anavyosema tutende haki, tupendane. Mfano wa Kaini ni chuki ambapo kupitia kwa huo mfano tunakumbushwa  tusiwe na chuki bali tupendane kama lilivyo agizo la Kristo Yesu. Mpende jirani yako kama nafsi yako. Amina

Siku njema

Heri Buberwa