Date
Reading
1 Yohana 2:12

Alhamisi asubuhi tarehe 01.10.2026;
1 Yohana 2:12
12 Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.
Tuwalee watoto katika njia ipasayo;
Asubuhi ya leo tunamsoma Yohana katika waraka wake akiandika juu ya amri mpya kwa Kanisa, yaani upendo. Ni katika kuhimiza upendo kwa waaminio, anawatia moyo watoto kwamba wamesamehewa dhambi zao kwa jina la Yesu.
Yohana anapowaambia watoto kwamba wamesamehewa dhambi zao, maana yake ni kwamba Mungu yuko nao, kwa hiyo waishi katika Kristo anayesamehe dhambi. Wito huu siyo kwa watoto tu, bali sote tukumbuke kwamba ni wenye dhambi tuliohesabiwa haki. Tusimuache Yesu aliyetusamehe, ili atufikishe kwenye uzima wa milele. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
