VIDEOS

Angalia picha mjongeo (Video) za ibada na matukio maalum ya Usharika hapa https://m.youtube.com/@AZANIAFRONTCATHEDRAL

Date
Reading
1 Timotheo 4:6-8

Alhamisi asubuhi tarehe 29.10.2026;

1 Timotheo 4:6-8

6 Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.

7 Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.

8 Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.

Mwenye haki ataishi kwa imani;
Paulo anamwandikia Timotheo yapasayo waamini kuishi kama watumishi wema wa Kristo Yesu. Anamwambia awafundishe kuhusu imani na mafundisho mazuri. Msisitizo wa Paulo kwa Timotheo ni kufundisha watu wakae katika neno la Mungu. Paulo anamsisitiza mwishoni Timotheo kudumu katika mafundisho sahihi na Kanisa kwa ujumla;

1 Timotheo 4:15-16

15 Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.

16 Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.

Neno la Mungu tunalolisikia kila siku lisipite tu, bali likae mioyoni mwetu, ndipo tutakuwa watumishi wema wa Kristo. Tujitunze nafsi zetu na kudumu katika neno la Mungu maana mwenye haki ataishi kwa imani. Amina

Siku njema

Heri Buberwa